Ni wapi naweza kufikia Double Up Food Bucks?
Ikiwa unaifahamu SNAP na unataka kujua zaidi kuhusu Double Up, unaweza kujifunza zaidi hapa:
Je, unajua kwamba unaweza kurudi nyumbani na kiasi maradufu ya matunda na mboga vibichi zilizokuzwa mahali hapo - na bila gharama ya ziada kwa familia yako?
Unapotumia kadi yako ya Oregon Trail EBT (pia inajulikana kama "SNAP" au "stempu za chakula" ) katika masoko ya wakulima na maduka ya vyakula yanayoshiriki, mpango ya SNAP Double Up Food Bucks huongeza maradufu kila dola unayotumia. Mpango huu unatumika katika maeneo mengi kote Oregon, ikijumuisha maduka yanayomilikiwa na watu binafsi ambayo hutoa aina mbalimbali za vyakula vinavyojulikana kitamaduni na vya kitamaduni. Unaweza hata kutumia Double Up kwa punguzo kuu kwenye hisa ya mavuno ya uanachama wako wa kila mwaka wa CSA!
Nyenzo hii inaangazia manufaa ya SNAP Double Up Food Bucks kwa wakazi wa Oregon. Unaweza pia kutumia manufaa yako ya Oregon SNAP EBT kupata matunda na mboga zaidi katika maeneo haya ya Washington au Idaho.
Ikiwa unaifahamu SNAP na unataka kujua zaidi kuhusu Double Up, unaweza kujifunza zaidi hapa:
Ikiwa unatafuta maduka ya karibu na masoko ya wakulima ambayo yanakubali Double Up, ramani hii ya kutafutika inaweza kusaidia:
Iwapo huna uhakika kama umehitimu kupata manufaa, hiki hapa ni zana muhimu unayoweza kutumia ili kuona kama unastahiki:
Ikiwa una maswali zaidi kuhusu SNAP Double Up Food Bucks au jinsi programu inaweza kusaidia familia yako, endelea kusoma!
Tumia tokeni au kuponi za Double Up ili kupata ulinganisho wa dola kwa dola ya hadi $20 ya kutumia kununua matunda, mboga au mbegu/mizizi ya mboga.
Uliza mfanyakazi katika duka la chakula linaloshiriki kujifunza jinsi unavyoweza kutumia Double Up katika eneo hilo. Katika maduka ya vyakula, unaweza kupokea Double Up yako kupitia kuponi, kadi ya duka au punguzo la moja kwa moja.
Baada ya kujaza fomu fupi, Double Up Food Bucks inaweza kutumika moja kwa moja kwa agizo lako la mazao, kwa kutumia kadi yako ya Oregon Trail ya manufaa ya chakula cha SNAP.
Imechukuliwa kutoka kwa muundo wa kitaifa wa Fair Food Network, Oregon Double Up Food Bucks hurahisisha wakazi wa Oregon wa kipato cha chini kula matunda na mboga zaidi huku wakisaidia wakulima wa familia na uchumi wa mitaa. Double Up ni mpango ya kwanza wa kusisimua wa jimbo lote la Oregon, ililyoundwa ili kuwafaa wanunuzi. Mpango huu huongeza maradufu thamani ya Mpango wa Usaidizi wa Lishe ya Ziada (wakati fulani huitwa "SNAP" au "stempu za chakula") katika masoko ya wakulima, maduka ya vyakula, na mashamba ya CSA (Kilimo Kinachoungwa mkono na Jamii) yanayoshiriki ili wanunuzi waweze kurudi nyumbani na mazao zaidi zilizotoka shambani. Double Up kwa sasa inatolewa katika zaidi ya maeneo 85 ya soko za wakulima, maduka 35 ya vyakula na zaidi ya mashamba 40 ya CSA kote jimboni - huku maeneo mapya yakijiunga na mpango huo kila mwaka.
Mpango wa Usaidizi wa Lishe ya Ziada (SNAP) ni mpango unaofadhiliwa na serikali kwa ajili ya kununua chakula wakati mapato ni ya chini. Manufaa yanapakiwa kwenye kadi ya SNAP EBT, wengine pia huitaja kama "Oregon Trail Card". Kadi hufanya sawa na kadi ya malipo, lakini pesa inaweza tu kutumika kwa bidhaa za chakula.
Kadi ya EBT ya kila mtu ina kiasi tofauti cha pesa kinachoambatanishwa nacho kulingana na mapato yao ya kibinafsi na hali ya familia - hadi $234 kila mwezi kwa kaya ya mtu mmoja au $782 kwa familia ya watu wanne. Utapokea maelezo ombi lako litakapoidhinishwa. Kila mwezi uliojiandikisha katika mpango wa SNAP, kiasi hiki kitaongezwa kwenye kadi yako na kinaweza kutumika kununua chakula. Pesa zozote ambazo hazijatumika zinapatikana kwa hadi mwaka mmoja kuanzia tarehe zitakapoongezwa kwenye kadi yako.
Zaidi ya hayo, maduka mengi na masoko ya wakulima hushiriki katika mpango wa Double Up Food Bucks kwa wapokeaji wa SNAP, ambao wanalinganisha hadi $20 kila siku kwa ununizi wa matunda na mboga zinazokuzwa mtaani. Wenye kadi za SNAP wanaponunua matunda na mboga vibichi katika maduka yanayoshiriki, masoko ya wakulima na washirika wa chakula wanapata $1 kwa Double Up kwa kila $1 wanayotumia katika SNAP. Bofya hapa kwa ramani ya kutafutika kwa msimbo wa zip, ya maduka yanayoshiriki.
Katika maduka ya vyakula, Double Up inaweza kutumika kununua:
Matunda na Mboga Vibichi
Mimea Vibichi
Uyoga
Mizizi za Mboga, Mimea au Matunda
Mbegu za Mboga, Mimea au Matunda
Katika masoko ya wakulima, Double Up inaweza kutumika kwa:
Matunda na Mboga Vibichi
Mimea Vibichi
Matunda na Mboga zilizogandishwa na Kukaushwa
Uyoga
Maharage
Mizizi za Mboga, Mimea au Matunda
Mbegu za Mboga, Mimea au Matunda
Double Up haiwezi kutumika kwa:
Bidhaa yoyote ya matunda au mboga iliyoongezwa chumvi, sukari, au mafuta
Ex. Matunda au mboga za makopo, vifurushi vya saladi vilivyo na mchuzi, vikombe vya matunda au juisi zilizoongezwa sukari
Double Up Food Bucks inapatikana kwa watumiaji wote wa SNAP, bila kujali kadi yako inatoka wapi. Kwa mfano, wateja walio na kadi ya Washington SNAP wanaweza kutumia manufaa ya Double Up kwenye duka la chakula la Oregon au soko la wakulima. Pata maelezo zaidi kuhusu Double Up Food Bucks hapa.
Kumbuka kwamba kiasi cha fedha za msingi za SNAP unazopokea zinatokana na mapato yako na idadi ya watu katika kaya yako - watu unaoshiriki nao ununuzi wa chakula. Lakini kila mtu anastahiki ulinganisho wa juu kabisa ya Double Up, kulingana na eneo unalofanya ununuzi. Tazama ukurasa wetu wa rasilimali kwa maelezo ya ziada kuhusu miongozo ya ustahiki wa SNAP.
Double Up Food Bucks inawezekana kupitia ushirikiano kati ya Oregon Food Bank, Mikopo ya Soko ya Wakulima (Farmers Market Fund), Muungano wa CSA wa Pasifiki ya Kaskazini-Magharibi (Pacific Northwest CSA Coalition), na Ushirika wa Wakulima wa Oregon (Oregon Farmers Markets Association). Kwa pamoja tunaunga mkono Double Up katika zaidi ya maeneo 85 ya soko za wakulima, maduka 35 ya vyakula na zaidi ya mashamba 40 katika jimbo lote.
Wafadhili wetu binafsi, wakfu na jumuiya wameturuhusu kukua na kuwa shirika linalostawi katika jimbo lote linalohudumia maelfu ya wanajamii wenye kipato cha chini na chakula chenye lishe kutoka kwa wakulima wa mitaa na wazalishaji wa chakula. Double Up pia inaungwa mkono na Programu ya Gus Schumacher ya Ushawishi wa Kusisimua ya Lishe nambari 2020-70030-33183 / 1024374 na 2022-70415-38570 / 1029309 kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Chakula na Kilimo ya USDA - pamoja na Programu ya Gus Schumacher ya Ushawishi wa Kusisimua ya Lishe Msaada wa Covid na Majibu Nambari 2021-70034-35369 / 1027071.
Unaweza kutumia Dola za Double Up unaponunua bidhaa zinazostahiki katika maduka ya vyakula yanayoshiriki katika jimbo lote. Tumia tu kadi yako ya SNAP EBT kwenye duka la chakula linaloshiriki na ununue matunda na mboga vibichi uvipendavyo. Kwa kila $1 katika SNAP unayotumia, utapata $1 ya Double Up Food Bucks ili utumie kwa matunda na mboga vibichi zaidi, hadi $20 kwa kila ununuzi. Katika maduka ya vyakula, unaweza kupokea Double Up yako kupitia kuponi, kadi ya duka au punguzo la moja kwa moja. Uliza keshia au mfanyakazi katika duka linaloshiriki kujifunza jinsi ya kupata Double Up katika eneo hilo. Maelezo ya ziada kuhusu jinsi ya kutumia Double Up katika duka la chakula yanapatikana kwenye tovuti ya Double Up Food Bucks.
Unaweza kutumia Dola za Double Up unaponunua bidhaa zinazostahiki katika masoko ya wakulima yanayoshiriki katika jimbo lote. Tumia tu kadi yako ya SNAP EBT kwenye soko la wakulima linaloshiriki na utembelee kibanda cha taarifa kabla ya kuanza ununuzi. Kwa kila $1 katika SNAP unayotumia, utapata $1 ya Double Up Food Bucks ili utumie kwa matunda na mboga vibichi zaidi, hadi $20 kwa kila ununuzi. Kwa mfano: ukitumia $20 katika manufaa ya SNAP, utapata $20 ya ziada bila malipo ambayo unaweza kutumia kununua bidhaa zaidi.
Katika masoko mengi ya wakulima, kila moja ya tokeni/kuponi za Double Up zina thamani ya $2, kwa hivyo kununua idadi shufwa cha dola kwa manufaa ya SNAP huhakikisha kuwa unaweza kupata ulinganisho kamili. Kwa mfano: ukitumia $5 katika SNAP kwenye ununuzi wako, utapata tu $4 katika Double Up; lakini ukitumia $6 kwa SNAP, utapata $6 kamili kwa Double Up.
Jumla ya ulinganisho ya kila siku ya Double Up inatofautiana kulingana na eneo la soko la wakulima. Tazama orodha kamili ya maduka ya vyakula, masoko ya wakulima na CSAs zinazoshiriki, ili kujua kikomo cha ulinganisho za kila siku unaponunua. Maelezo ya ziada kuhusu jinsi ya kutumia Double Up katika soko la wakulima yanapatikana kwenye tovuti ya Double Up Food Bucks.
Programu za CSA ni kama usajili wa jarida, lakini kwa chakula! Kila wiki mkulima wako atakuletea aina mbalimbali za vyakula vibichi na vyenye lishe kwenye maeneo karibu nawe. Unapotumia manufaa ya chakula cha SNAP kupitia Kadi yako ya Oregon Trail kununua CSA/hisa ya mavuno kutoka kwa shamba linaloshiriki, Double Up Food Bucks itatumwa moja kwa moja kwa malipo yako. Kunaweza kuwa na fomu fupi ya kutia saini na kurudisha kwa njia ya posta, lakini mchakato wa jumla ni nyepesi na rahisi. Maelezo ya ziada kuhusu jinsi ya kutumia Double Up kwa CSA yanapatikana kutoka Muungano wa CSA wa Pasifiki ya Kaskazini-Magharibi.
Tumeweka watu wanaokabiliwa na njaa katikati ya kila uamuzi tunaofanya.
Mipango kama vile Double Up Food Bucks ni muhimu sana ili kuhakikisha sote tunapata chakula bora. Lakini miongo kadhaa ya uzoefu inatuambia kwamba msaada wa chakula pekee bado hautoshi kumaliza njaa milele. Ndio maana tunafanya kazi kwa bidii kubadilisha sera na mifumo inayosababisha njaa katika jamii zetu. Jisajili kwa arifa za hatua ili ujifunze jinsi unavyoweza kuhusika katika mapambano ya kuondoa njaa kwenye chanzo chake.
Kwa mujibu wa sheria ya shirikisho ya haki za kiraia na sheria na sera za haki za kiraia za Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA), taasisi hii hairuhusiwi kubagua kwa misingi ya mbari, rangi, asili ya kitaifa, jinsia (ikiwa ni pamoja na utambulisho wa kijinsia na mwelekeo wa kijinsia), imani ya kidini, ulemavu, umri, imani za kisiasa, au kulipiza kisasi kwa kuhusika katika shughuli za awali za haki za kiraia.
Maelezo ya mpango yanaweza kupatikana katika lugha zingine isipokuwa Kiingereza. Watu wenye ulemavu wanaohitaji njia mbadala za mawasiliano ili kupata maelezo ya mpango (km, Breli, maandishi makubwa, kanda ya sauti, Lugha ya Ishara ya Marekani), wanapaswa kuwasiliana na shirika (la jimbo au eneo) ambako walituma maombi ya msaada. Watu ambao ni viziwi, walio na matatizo ya kusikia au walio na matatizo ya kuzungumza wanaweza kuwasiliana na USDA kupitia Huduma ya Uelekezi ya Shirikisho (Federal Relay Service) katika (800) 877- 8339.
Ili kuwasilisha malalamiko ya ubaguzi katika mpango, Mlalamishi anapaswa kujaza Fomu ya AD-3027, Fomu ya Malalamiko ya Ubaguzi wa Mpango wa USDA ambayo inaweza kupatikana mtandaoni katika: https://www.fns.usda.gov/sites..., au kutoka ofisi yoyote ya USDA, kwa kupiga simu (833) 620-1071, au kwa kutuma barua kwa USDA. Barua lazima ijumuishe jina, anwani, nambari ya simu ya mlalamishi, na maelezo ya maandishi ya madai ya kitendo cha ubaguzi kwa undani wa kutosha ili kumfahamisha Katibu Msaidizi wa Haki za Kiraia (ASCR) kuhusu asili na tarehe ya madai ya ukiukaji wa haki za kiraia. Fomu au barua iliyojazwa ya AD-3027 lazima iwasilishwe kwa:
1. barua:
Food and Nutrition Service, USDA
1320 Braddock Place, Room 334
Alexandria, VA 22314; au
2. faksi:
(833)-256-1665 au (202)-690-7442; au
3. barua pepe:
FNSCIVILRIGHTSCOMPLLAINTS@usda.gov
Taasisi hii ni mtoa huduma asiyebagua.
Sign up to receive emails with updates, resources and ways to get involved.